Na Ichikael Malisa - Njombe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango ametoa rai kwa vijana kufanya kilimo cha parachichi ili kujikwamua kiuchumi.
Mheshimiwa Mpango ametoa rai hiyo Oktoba 26,2023 mjini Makambako alipofanya ziara kwenye kiwanda cha kusindika zao la parachichi cha AvoAfrica.
Akiwa kiwandani hapo amesema uwekezaji mkubwa uliofanyika una faida kubwa kwa wananchi wa njombe na Tanzania nzima, kwa kutoa ajira na kuongeza pato la taifa.
"Niwapongeze uwekezaji huu, watanzania wenzangu tumepewa fursa kubwa dhahabu ya kijani ni fursa hasa kwa vijana, hakuna haja yakukaa mtaani changamkieni fursa,Wafanyakazi tumieni f vizuri fursa ya ajira mliyoipata nanyi muwe na mashamba yenu." Alisema.Mhe Mpango
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais Mheshimiwa Mpango, ametaka mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuhakikisha inaondoa vikwazo visivyo vya lazima vinavyopelekea ucheleweshaji wa shehena za parachichi ili kuwezesha parachichi kufika kiwandani kwa wakati unaotakiwa.
Aidha amewaomba wananjombe kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambayo inapambana kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na maisha bora.
Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika kwenye kiwanda hicho Mheshimiwa makamu wa raisi ametoa rai kwa wanahabari kutangaza fursa ya kilimo cha parachichi kwa vijana.
"Hiki kiwanda ni cha mfano wanahabari, tangazeni haya ili vijana wengi waweze kuchangamkia fursa hii ya kilomo cha parachichi."
Ili kulinda soko la parachichi kimataifa mheshimiwa makamu wa Rais amewakumbusha wakulima kuhakikisha wanachuma matunda yaliyokomaa kama wanavyoshauriwa na wataalamu.
Uwekezaji wa kiwanda cha parachichi cha AvoAfrica mjini Makambako unatajwa kugharimu dola za kimarekani takribani milioni 4.8.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe