Kikundi kinachojihusisha na shughuli za utunzaji na uhifadhi wa mazingira cha Wildfire and Restorartion Organization (WFRO) kilichopo kata Uwemba,Juni 17,2024 kimekabidhiwa mizinga 10 yenye thamani ya shilingi 708,000.00 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2024 Ndg. Godfrey Mnzava iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua msitu wa Isililo wenye ukubwa wa hekta 58.88 ambapo kikundi hicho kina jumla ya mizinga mitano (05) ambayo imetundikwa ndani ya Msitu,ikiwa ni kuunga mkono jitihada za vijana hao katika uhifadhi wa mazingira.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amewapongeza vijana hao nakuwaasa kuendelea kufanya kazi zinazohifadhi mazingira na mabalozi wa utunzaji wa mazingira kwa watu wengine ili kuepuka athari za muda Mrefu zinazotokana na uharibifu wa mazingira.
Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2024 zinaongozwa na kauli mbiu isemayo "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu ".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe