Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amewataka Wakala wa barabara Nchini TANROAD pamoja na Wakala la wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA Mkoa wa Njombe kutoa Kipaumbele kwa barabara zinazoelekea maeneo yenye Shughuli za uzalishaji, Miradi ya Maendeleo na Huduma za Jamii ili kuharakisha Maendeleo katika maeneo hao.
Akizungumza katika kikao Cha Bodi ya Barabara kilichofanyika leo Mtaka amesema kuwa ni vyema Taasisi Hizi kuja na Mpango kabambe wa ujenzi wa barabara yaani "Master Plan" utakaoonyesha namna miundombinu ya barabara itakvyoweza kuwafikia Wananchi na kufikia maeneo ya kiuzalishaji na kimkakati
Awali Katibu tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omary amesema kuwa Mkoa wa Njombe unajumla ya Kilometa 1188 za barabara zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) na Kilometa 5200 zinahudumiwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura).
Katika taarifa yake Meneja wa Tanroads Mkoa wa Njombe Mhandisi Lucy Shalua amesema wanaendelea na ujenzi wa barabara mbalimbali ambapo jumla ya KM 107.4 zimekamilika na zipo kwenye matazamio.
Meneja wa Tarura Mkoa wa Njombe Mhandisi Gerlad Matindi amesema kuwa wamepokea kiasi Cha shilingi Bilioni 20.34 kwa ajili ya matengenezo ya barabara na kiasi Cha shilingi Bilioni 16 zimeshatumika.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe