Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe,Balozi Dkt, Pindi Chana amesema kuwa vivutio vya Utalii ambavyo ni vizuri na vya Kipekee vinavyopatikana katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania ni fursa kwa Wananchi wa Mikoa hiyo kunufaika na kujiongezea kipato kutokana na uwepo wa vivutio hivyo.
Waziri Chana ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yaliyohudhuriwa na wadau kutoka katika Mikoa kumi ambayo ni Iringa,Njombe, Mbeya,Ruvuma,Mtwara,Lindi,Morogoro,Rukwa,Katavi na Songwe ambapo yamezinduliwa leo Mkoani Iringa.
Akizungumza katika uzinduzi huo Dkt,Chana amesema kuwa ni vyema wadau mbalimbali kuendlea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutangaza vivutio hivyo vya utalii vilivyopo katika Mikoa hiyo kutokana na upekee wa vivutio hivyo
Aliendelea kusema kuwa mpaka sasa kufikia mwezi Septemba 2022,idadi ya Watalii imeongezea na kufikia 1,034,180 kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutangaza Utalii kupitia filamu ya The Royal Tour,ambayo imeleta neema ya ujio wa Watalii wengi Nchini
Maonesho hayo ambayo yataendelea kwa muda wa siku tano ambapo Wananchi wanakaribishwa ili kuweza kujionea na kupata taarifa za vivutio vilivyopo katika Mikoa hiyo ambapo Halmashauri ya Mji Njombe nayo inashiriki pamoja na Halmasahuri zote za Mkoa wa Njombe kutangaza vivutio vyao
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe