Waandikishaji wa wapiga Halmashauri kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Tarehe 07 Oktoba 2024 wamepatiwa semina maalum ili kuwaelimisha na kuwaandaa kwa ajili ya zoezi la uandikishaji wa wapiga kura linalotarajiwa kuanza Tarehe 11 - 20 Oktoba 2024.
Katika semina hiyo, waandikishaji wamehimizwa kufanya kazi kwa uadilifu na umakini mkubwa. Wawezeshaji wa semina walisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anayestahili kuandikishwa kama mpiga kura anapata haki yake bila ubaguzi wowote.
Waandikishaji walikumbushwa kuwa kazi yao ni ya msingi katika kuimarisha demokrasia, hivyo wanapaswa kuwa waaminifu katika utekelezaji.
Aidha, walielekezwa kuhusu umuhimu wa kuzingatia muda wa kazi. Ilisisitizwa kuwa waandikishaji wanapaswa kuwa kwenye vituo vyao vya kazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni bila kukosa ,ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata nafasi ya kuandikishwa kwa wakati uliopangwa ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu ucheleweshaji au upotevu wa haki yao ya kuandikishwa.
Msimamizi msaidizi Ndg.Dotto Kulaba aliyekuwa mwezeshaji mkuu, aliwahimiza waandikishaji kuhakikisha kuwa wanatoa huduma kwa wananchi kwa weledi, uvumilivu, na kuwahudumia kwa haraka na usahihi. Alisisitiza kuwa mchakato huu ni nyeti na unahitaji umakini mkubwa ili kuhakikisha taarifa zote za wapiga kura zinasajiliwa kwa usahihi bila makosa.
Semina hii imewapa waandikishaji uelewa mzuri wa majukumu yao, na ni hatua muhimu katika maandalizi ya mchakato wa uandikishaji wa wapiga kura.
"Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe