Waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki katika zoezi la uboreshaji wa daftari la Kudumu la wapiga kura Jimbo la Njombe Mjini,wameaswa kutunza vifaa sambamba na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, bidii na kujituma ili kazi hiyo iweze kuwa bora.
Wito huo umetolewa Januari 09 mwaka huu na Afisa mwandikishaji Jimbo la Njombe mjini, Samson Medda wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Amejimiza ushirikiano na kusema kuwa ili kuweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi wanapaswa kuwa na bidii na moyo wa kujituma ili kuhakikisha zoezi hilo la kitaifa linafakiwa kwa kiasi kikubwa.
“Ni muhimu kuwepo kwa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wote wa uchaguzi, pamoja na kuvitunza vifaa vyote vitakavyotumika katika uboreshaji na kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na tume,” Amesema Medda.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Asina Omari amesema mafunzo hayo ni tofauti na mafunzo mengine kwa sababu yanawawezesha kwenda kufanya kazi na kuonya lugha mbaya kwa wananchi pindi wanapofika katika vituo kujiandikisha.
Mafunzo hayo yaliambatana na kiapo kilichoongozwa na Kamishna wa Viapo Hakimu Isaack Romanus Mlowe, ambapo watendaji hao waliapa kiapo cha kutunza siri na kujivua uanachama wa chama cha siasa ili zoezi hilo liweze kufanyika kwa uwazi na haki.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga Kura Jimbo la Njombe Mjini litafanyika Tarehw 12 - 18 Januari 2024 na vituo vya uandikishaji vitakuwa wazi Saa 2 Asubuhi hadi saa 12 jioni.
"Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora ".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe