Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe Erasto Mpete amewaomba Wadau wa Maendeleo, Wananchi na Taasisi mbalimbali kuchangia ujenzi wa Shule shikizi ili kuwapunguzia adha wananchi na Wanafunzi wanaoishi eneo la Block (X) lililopo kata ya Njombe Mjini.
Mhe Mpete ametoa rai hiyo Oktoba 10,2023 alipotembelea eneo hilo la Block (X) ambalo litajengwa Shule Shikizi itakayokuwa na vyumba vya Madarasa vitatu (3) Ofisi moja (1) na Matundu ya vyoo Nane (8).
Mhe Mpete amesema ametembelea Eneo hilo kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi wa mtaa huo kuhitaji kutatua changamoto iliyopo kwenye eneo lao ambapo kwa jitihada za wananchi Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe imetoa kibali cha ujenzi wa Shule shikizi katika eneo hilo.
" Niwaombe wananchi,Taasisi mbalimbali na wadau wa Maendeleo kuweza kuchangia Ujenzi wa Shule hii ili kwa pamoja tuweze kupunguza changamoto kwa watoto wetu wanaotembea umbali mrefu,Hivyo tunaomba watu wetu walioteuliwa kuchangisha mchango wa Ujenzi wakipita kuomba mchango wa kuchangia ujenzi huu tusisite kutoa,na ambaye anaweza kutoa chochote tunaomba atusaidie kama vile Mchanga au mawe ili Tukamilishe kwa wakati"Alisema Mhe Mpete.
Kwa Upande wake Amosi Luhamba Afisa Mipango miji wa Halmashauri ya Mji Njombe amesema Eneo hilo lina ukubwa wa Ekari 1.8 na ujenzi wa Kituo hicho utawasaidia wananchi wa mtaa huo kutatua changamoto na kuwalinda watoto wao huku akitoa ombi kwa wananchi wa mtaa huo kuhakikisha wanatunza mazingira kwa Kupanda Miti ambayo itasaidia kuongeza hewa safi.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Njombe mjini Enos Lupimo amesema wamejipanga kuhakikisha ujenzi wa shule hikizi unaenda kwa kasi kubwa huku akisisitiza wananchi kuunga mkono ujenzi huo.
Ujenzi wa Shule Shikizi ya mtaa wa Block (X) utapunguza changamoto ya wanafunzi wa eneo hilo kuacha kutembea umbali mrefu na kuacha kupita kwenye maeneo hatarishi ikiwemo barabara kuu ya Songea wakati wa kwenda shule Jirani za Mji mwema,Nazarèth na Sabasaba.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe