Mkuu wa Mkoa Njombe Mhe Anthony Mtaka amewashukuru wadau na wanunuzi wa parachichi kwa kuchangia kiasi cha shilingi Milioni 14. 5 kwa ajili ya kusaidia kampeni ya kutokomeza Udumavu Mkoani Njombe
Mhe.Mtaka ametoa shukrani hizo Januari 15,2024 alipokutana na kuzungumza na wadau hao ofisini kwake kuhusu mwenendo wa zao la parachichi katika soko la ndani na kimataifa, kujadili changamoto mbalimbali wanazo kabiliwana nazo wakulima na wanunuzi wa parachichi ,muda wa kuanza kuchuma parachichi shambani pamoja kujadili fursa juu ya zao la parachichi ambalo ni dhahabu ya kijani katika Mkoa wa Njombe.
Katika kikao Hicho Mhe Mtaka amewapongeza wadau hao kwa uzalendo nakuona umuhimu wakuchangia katika kampeni ya kutokomeza udumavu katika Mkoa wa Njombe.
Aidha Mhe Mataka amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya Tanzania kuja kuwekeza kwa wingi kwenye viwanda vya kuongeza thamani katika zao hilo ili kuweza kuongeza ushindani katika soko la ndani na kimataifa kutokana na parachichi ya Njombe kuwa bora katika soko la kimataifa hasa falme za kiarabu na China ambako Mhe Rais Samia Suluhu Hassan alitembelea kutafuta masoko na fursa za uwekezaji katika zao hilo.
Naye Meneja wa Kampuni ya Ununuzi wa Parachichi Mkoani Njombe Avo Africa Nagib Karmal ambaye aliteuliwa katika kikao hicho kuongoza kampeni ya uchangishaji kwa wadau hao amesema wanunuzi na wadau wa parachichi Mkoani Njombe wameamua kuchangia shilingi milioni 14.5 katika kampeni ya lishe kutokana na hali ya Lishe Mkoani Njombe kuwa mbaya nakupelekea Mkoa kuwa na asilimia kubwa ya Watoto waliodumaa jambo ambalo limewaibua mpaka viongozi wa Nchi kulivalia njuga.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe