Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Selelamani Mtibora, amewataka wadau mbalimbali wa Uchaguzi Mkoani Njombe, kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.
Akizungumza Desemba 31, 2024, kwa niaba ya Mwenyekiti wa INEC, Jacobs Mwambegele, Mtibora alisisitiza umuhimu wa wadau kutumia majukwaa mbalimbali ya kisiasa, kijamii, kitamaduni, kiimani, na kiuchumi ili kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
Mtibora alieleza kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mkoa wa Njombe litaanza rasmi Januari 12, 2025. Aliwataka wapiga kura ambao kadi zao hazijapotea, hazijaharibika, hawajahama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda jingine, au taarifa zao hazijakosewa, kufika kwenye maeneo yaliyotengwa kwa uboreshaji wa daftari hilo ili kupokea maelekezo muhimu.
Hadi sasa, zoezi la uboreshaji limekamilika katika mikoa 19, ambapo wananchi wa maeneo hayo wameshaandaliwa kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Zoezi hili linaendeshwa chini ya kaulimbiu isemayo: "Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi bora".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe