Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) na kuwakabidhi vyeti wahitimu 84 waliokamilisha mafunzo hayo. Hafla hiyo imefanyika Agosti 19, 2025 katika Uwanja wa Sabasaba, Njombe.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Sweda aliwapongeza wahitimu kwa uvumilivu na nidhamu waliyoonesha kipindi chote cha mafunzo, huku akiwataka kuendelea kudumisha uzalendo, mshikamano na kuepuka vitendo vya vurugu vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi.
Aidha, alisisitiza kuwa Jeshi la Akiba ni chombo muhimu katika kulinda amani na usalama wa taifa, hivyo kila mhitimu anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii zao.
Kwa upande wake, Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Njombe, Bw. Hussein Athumain Mchomvu, alisema kati ya wahitimu hao 84, wanaume ni 55 na wanawake 29. Alibainisha kuwa walipatiwa mafunzo mbalimbali yakiwemo ukakamavu wa mwili, mbinu za kivita, usomaji wa ramani, uraia pamoja na ujasiriamali.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe