Vikundi vya Ujasiriamali kutoka katika Mkoa wa Njombe Halmashauri ya Mji Njombe wametembelea katika banda la Mkoa wa Morogoro ambapo wamejifunza mbinu mbadala na za kisasa za utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na ufumaji na ususi kwa kutumia nyuzi.
Akizungumza akiwa ameambatana na Wajasiriamali kutoka Halmashauri ya Mji Njombe, Christina Daniel Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Njombe amesema kuwa lengo la wao kutembelea katika banda la Mkoa wa Morogoro Wilaya ya Ifakara ni kupata elimu na mbinu zaidi ya kuboresha bidhaa kwa Wajasiriamali wa Njombe na kujifunza Teknolojia mpya ambazo zinaweza kutumiwa na Wajasiriamali wa Njombe ili kuwa na bidhaa zenye ushindani katika soko.“Nimekutana na Wajasiriamali kama sisi ambao wanatoka Halmasahuri ya Mji Ifakara amabo nao ni Wanufaika wa asilimia kumi ya Mkopo wa Wanawake,Vijana na Walemavu. Nimeona niwalete Wajasiriamali wetu hapa ili waweze kujifunza vitu tofauti.Ningependelea vikundi vyetu vya Njombe vikajifunza utengenezaji wa bidhaa hizi kwani hizi ni bidhaa za viwanda na sisi tunapenda kwenda kwenye viwanda.”Alisema Christina.
Jonosia Malizi ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Liwa kutoka Halmashauri ya Mji Ifakara Morogoro, ambaye yeye ameseama kikundi chao kinatengeneza bidhaa mbalimbali kama vitambaa vya mezani,jikoni,blanketi,vikoi, ambao vimekuwa na manufaa makubwa katika kukuza uchumi wao. Jonosia amesema kuwa katika kutengeneza bidhaa zao na wamekuwa wakitumia nyuzi za mbao na mashine za mbao ambazo zinatengenezwa na mafunzi seremala ambapo mashine hizo hutengeneza mashuka na vikoa vine hadi vitatu kwa siku kazi ambayo inafanywa na mtu mmoja ambapo awali iliwalazimu kutumia mwezi kutengeneza bidhaa hizo.
Aidha Jonisia amesema kuwa licha ya kutengeneza bidhaa hizo pia kikundi hicho kinatoa elimu ya ufundi kwa Wanavikundi na wanafunzi wanaopenda kufanya shughuli za Ujasiriamali jambo ambalo linawaongezea kipato kupitia mafunzo hayo.
Nao Wajasiriamali kutoka katika Halmashauri ya Mji Njombe waliotembelea banda hilo na kijionea bidhaa hizo wamefurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Wanavikundi wenzao na wamesema kuwa teknolojia ya kutumia mashine imesaidia kurahisisha shughuli za uzalishaji wa bidhaa na wao pia watajipanga kutembelea na kujifunza kwa vitendao shughuli za uzalishaji wa bidhaa hizo ili waweze kuileta Teknolojia hiyo Njombe jambao ambalo pia litakuwa na mafufaa kwao lakini pia litawawezesha mafundi Seremala kupata ubunifu mpya wa kutengenza mashine hizo za ufumaji.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe