Wanafunzi wa kozi ya 12 kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa (National Defence College) Dar es salaam wanaofanya ziara yakujifunza kwa vitendo Mkoani Njombe, Januari 15,2014 wametembelea msitu wa Litoni (Litoni Forest Reserve) uliopo kijiji cha Nundu kata ya Yakobi, Halmashauri ya Mji Njombe.Wanafunzi hao kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Zambia, Namibia, Kenya China na India, pamoja na mambo Mengine wamejifunza namna Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) unavyohudumia msitu huo ambao una ukubwa wa hekari 200 kwa ajili ya uhifadhi wa vyanzo vya maji pamoja na misitu mingine inayopatikana ndani Wilaya ya Njombe.
Asilimia 45 ya Msitu wa Litoni unaundwa maeneo ya miinuko yenye milima midogo na mabonde ambamo vinapatika vyanzo mbalimbali vya maji vinavyounda mito mitatu ambayo ni mto Litoni, Mafowono na Mangohera ambayo inatiririsha maji yake mto rufiji nakuwa sehemu ya mito inayochangia maji kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere.
Aidha wamejifunza namna ambavyo mipak a ya msitu huo inavyolindwa pamoja na shughuli nyingine zinazofanywa na wakala ikiwemo kuhamasisha upandaji wa miti ili kutunza mazingira na kupunguza wananchi wanaovamia misitu kwa ajili ya kukata miti yakuzalisha nishati na matumizi mengine, matumizi sahihi ya ardhi, utunzaji shirikishi wa misitu kuzuia uchomaji wa misitu, pomoja mpango wakufanya ukaguzi kwenye misitu kwa njia za kidigitali
Awali Audatus Kashamakula Afisa Uhifdhi Wilaya ya Njombe alieleza kuwa Wakala unaendelea kushirikina na wananchi katika uhifadhi na unatoa shukrani jamii ya Njombe kwa mwitikio mkubwa kwenye uhifadhi, ambao umepunguza shughuli za kibinadamu kwa kiasi kikubwa kwenye misitu pamoja na kupunguza visa vya kuchoma moto misitu hadi kufikian asilimia 10 kwa kipindi cha mika miwili iliyopita.
Wanafunzi hao watatembelea maeneo mbalimbali mbalimbali kwenye Halmashauri za Mkoa wa Njombe kwa Lengo la kujifunza kwa vitendo na kujenga uelewa kuhusu Mkoa wa Njombe katika nyanja za kijamii kisiasa na kiuchumi katika maendeleo ya Nchi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe