Timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Dawa na vifaa Tiba (TMDA) kanda ya nyanda za juu kusini imeanza kutoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa kwenye Shule za Sekondari zilizopo Halmashauri ya Mji Njombe.
Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpechi Mkaguzi wa Dawa kutoka TMDA Bi Grace Kapande ametoa rai kwa wanafunzi hao kuwa mabalozi wa kufikisha elimu waliyopatiwa kwa jamii ili jamii itambue kuwa ,matumizi yoyote ya dawa yanapaswa kufanyika kwa kuzingatia ushauri kutoka kwa wa wataalamu wa afya.
Aidha ameeleza kuwa matumizi ya dawa yanapaswa kuzingatia na kufuata maelekezo sahihi ya kanuni za afya ili kupunguza madhara yatokanayo na matumizi holela ya dawa ikiwemo kutengeneza usugu na magonjwa kushidwa kutibika na kusababisha uharibifu wa viungo vya mwili kama figo.
Elimu hiyo itatolewa kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari kwa siku tatu kuanzia Oktoba 18,2023 hadi Oktoba 21,2023 katika Shule za Sekondari Mpechi,Yakobi ,Uwemba,Mbeyela na Mabatini.
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) ni taasisi ya serikali iliyopo chini ya wizara ya afya ,maendeleo ya jamii ,jinsia wazee naa watoto yenye jukumu la kudhibiti ubora ,usalama na ufanisi wa dawa ,vifaatiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe