Kuelekea Kilele cha maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani tarehe 24 Machi 2024, zaidi ya wananchi 300 wa kijiji cha Mamongolo kata ya Makowo Halmashauri ya Mji Njombe wamepatiwa elimu ya kifua kikuku (TB).
Akizungunza Machi 20,2024 wakati akitoa elimu katika kijiji hicho Dkt.Mashaka Kisulila Mratibu wa kifua kikuu Halmashauri ya Mji Njombe
amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanajitokeza kwenye vituo vya afya wanapopata dalili za kifua kikuu kutokana na ugonjwa huo kupoteza maelfu ya watu duniani.
Zoezi la kutoa elimu liliambatana na upimaji ambapo sampuli za makohozi na choo kutoka kwa watu 28 waliohisiwa kuwa na kifua kikuu zilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika Hospitali ya Mji Njombe(Kibena).
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe