Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Kasongwa amewataka wananchi wote mkoani Njombe kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) ambao umekuwa ukisumbua mamia ya watu nchini.
Akizungumza Machi 24,2024 kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani kwa Halmashauri ya Mji Njombe yaliyofanyika katika viwanja vya soko kuu Njombe amesema tafiti za Shirika la Afya Duniani zinaonesha kwa mwaka 2021 Tanzania ilikuwa na wagonjwa wakifua kikuu 133,000 hivyo ni muhimu kwa ,ila mwannachi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao ili kuepuka madhara makubwa yatokanayo na magonjwa mbalimbali mwilini.
Akitoa taarifa ya hali kifua kikuu kwa Halmashauri ya Mji Njombe , mratibu wa kifua kikuu Dkt.Mashaka Kisulila amesema kwa mwaka 2023 waliwekewa lengo lakuwafikia wagonjwa 333 na walifanikiwa kuvuka lengo hilo kwa asilimia 113.8 ambapo walifikia wagonjwa wa kifua kikuu wapatao 379 kati ya wagonjwa 1,650 waliobainika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu mkoani Njombe na kuwaanzishia matibabu.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe