Wananchi wa kijiji cha Miva kata ya Luponde Halmashauri ya Mji Njombe wametakiwa kutofumbia macho vitendo viovu vya ukatili wa kijinsia vinavyo tokea katika jamii.
Rai hiyo imetolewa Juni 19,2023 na Mkuu wa dawati la Jinsia na watoto wilaya ya Njombe Inspekta Mary Kweta alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha miva katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika Halmashauri ya Mji Njombe.
Inspekta Mary amewaasa wananchi wa kijiji hicho kuto kujichukulia sheria mkononi pale matendo maovu yanapojitokeaza ,badala yake watoe taarifa katika kamati za madawati ya jinsia zilizopo karibu na maeneo yao .
Akiendelea kuzungumza na wanachi hao Ispekta Mary Kweta ameisihi jamii kuhakisha inawajibika kutoa elimu ya vitendo vya ukatili kwa watoto na kuwafundisha mbinu mbalimbali zakujilinda.
Kwa upande wake Oddo Msemwa Afisa Maendeleo Halmashauri ya Mji Njombe amesema Halmashauri imejipanga kuhakikisha vitendo viovu vya ukatili kwa watoto vinakomeshwa kwa kuanzisha mabara ya watoto kwa ngazi ya vijiji na kata, dawati la ulinzi na usalama wa mtoto ndani na nje ya shule pamoja kuimarisha vikundi vya malezi ya watoto kwenye jamii .
Naye Petro Mahanza Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji Njombe ameomba wanawake na wanaume ambao wanafanyiwa ukatili na wenza wao na wanao kimbia malezi kwa watoto baada ya kuwazalisha wenza wao kuchuuliwa hatua
Nao wananchi washiriki kutoka kijiji cha Miva Faustin Mwalongo,Jofrey Kisswaga na Jorge Mgaya wameishukuru halmashauri ya mji njombe kwa kuwapa elimu juu ya ukatili ambayo itaenda kuwasaidia kuwaepusha watoto na vitendo viovu pamoja na kutoa taarifa kwa wakati pindi matatizo yanapojitikeza.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe