Septemba 20, 2025 Wananchi wa Mtaa wa Mgandela na National Housing wameungana kufanya usafi wa mazingira katika mitaa yao kwa kuokota taka, kufyeka vichaka na kusafisha maeneo ya wazi.Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Usafi wa Mazingira Duniani ambapo zoezi hilo litasaidia kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuzuia magonjwa yanayosababishwa na uchafu kwa wakazi wa maeneo hayo kuendeleza tabia ya kufanya usafi mara kwa mara ili mtaa ubaki safi na salamaKaulimbiu ya mwaka 2025 inasema “Tunza Mazingira kwa Kuzipa Taka Thamani”, ikihamasisha jamii kuona taka si uchafu tu bali rasilimali inayoweza kutumika kwa manufaa kama vile kutengeneza mbolea, nishati na bidhaa nyingine.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe