Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Isdor Mpango ameweka jiwe la Msingi kwenye mradi mkubwa wa maji kutoka chanzo cha maji kilichopo kata ya Lugenge Halmashauri ya Mji Njombe.
Mheshimiwa makamu wa Raisi amepongeza mamlaka ya maji NJUWASA kwa hatua zilizofikiwa kwenye ujenzi wa mradi huo wenye gharama ya shilling bilioni 8.7, ambao umekamilika kwa asilimia 82 huku ujenzi wa mtandao ukiwa umekamilika kwa asilimia 100.
Aidha ameielekeza Wizara ya maji chini ya waziri Jumaa Aweso kuhakikisha mradi huo pamoja na miradi mingine inakamilika kwa wakati, pia kuharakisha zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi wote waliopisha mradi.
"Hakuna kuchelewa, Serikali ya mama Samia imetoa fedha, fanyeni kazi usiku na mchana"
Katika hatua nyingine Dkt.Mpango amesema serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan haitolala usingizi mpaka kila mama aweze kupata maji nyumbani au jirani na nyumbani.
Kukamilika kwa mradi huo kutatatua changamoto ya maji mjini njombe kwa asilimia 85 na kuwa na uhakika wakutoa huduma kwa saa 24.
Dkt.Mpango ameweka jiwe la Msingi kwenye tenki moja kubwa la maji lenye ujazo wa Lita 500,000.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Isdor Mpango, alianza ziara mkoani Njombe Oktoba 26,2023 na atahitimisha kwa ziara yake kwa kufunga maonesho ya nne ya Viwanda Vidogo SIDO Oktoba 28,2023 kwenye viwanja vya sabasaba mjini Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe