Wanawake wametakiwa kutafuta maarifa yatakayowasaidia kuongeza kipato na kukuza uchumi kwenye familia zao.
Rai hiyo imetolewa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka Machi 08,2024 katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2024 yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Usita kata ya Ulembwe Wilayani Wanging’ombe.
"Familia yeyote ile ni uchumi mnapofundisha kwenye kitchen party fundisheni kuhusu kujitambua, suala la malezi kwa watoto na kufanya kazi kwa bidii, ili kuinua uchumi na ustawi wa familia. "Alisema Mhe. Mtaka.
Aidha amewataka wanawake walio kwenye vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana kuacha kukaa kwa mazoea na badala yake wafikiri namna ya kuongeza ujuzi na maarifa kwa kualika watu waliofanikiwa kwenye biashara kuwapatia elimu na uzoefu kwenye safari ya mafanikio ili uwepo wao kwenye vikundi uwe na tija katika kukuza uchumi wao.
Mhe. Mtaka amesisitiza kuwa wanawake ni msingi wa familia na ili kudhirihisha msemo wa ukimwelisha mwanamke umeielimisha jamii ni lazima wanawake wakubali kurudi kwenye msingi wa malezi bora kwa watoto.
"Mwanamke anauwezo mkubwa wa kumlea na kumjenga mtoto wa kike na wakaime, wanawake ni jeshi kubwa tengenezeni jeshi kubwa kwenye uchumu tumieni mkutano yenu ya wanawake kufundishana mambo ya msingi"Alisisitiza Mhe. Mtaka.
Amewataka vijana wakiume kuwekeza muda wao kufanya kazi zitakazowajenga kiuchumi bila kusahau kuhudummia familia zao haswa watoto kwa kuhakikisha wanapata lishe bora.
Katika hatua nyingine amewahamasisha wanawake kugombea nafasi za uongozi na kuwaunga mkono wanawake wengine watakaojitokeza kuwania nafasi hizo kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2024 inasema "Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe