Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva, katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2024 mkoani Njombe, amesema kaulimbiu ya mwaka huu inawataka wanawake na jamii kuwekeza kwa mabinti kwa kuhakikisha wanapata elimu.
Mhe. Mwanziva amewasisitiza wanawake kuendelea kuwekeza kwenye uchumi na kudumisha umoja wa kukaa kwenye vikundi na kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,anayepambana kuhakikisha taifa linakuwa kiuchumi.
Aidha amewataka wanawake kuwa bora kwenye maeneo yao ya kazi kufanya kazi kwa bidii, weledi na udilifu pamoja nakuendelea kujifunza ili kuleta heshima kwa nafasi walizoaminiwa kuzitumikia katika utumishi wa umma.
Sambamba na hayo amewakumbusha wanawake wote kuwa bora kwenye familia kwa kuzingatia lishe bora kwa watoto wao.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2024 inasema "Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe