Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, leo Machi 04,2024 wakazi Mjini Njombe wakiongozwa na wataalamu kutoka Idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya Mji Njombe, wameshiriki zoezi la kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali kuzunguka kituo cha afya Mjimwema.
Shughuli nyingine zitakazoendelea kufanyika kuelekea kilele Machi 08,2024 ni pamoja na mdahalo wa kuitafsiri kauli mbiu ya mwaka 2024 utakaofanyika Machi 05,2024 Shule ya Sekondari Anna makinda, maadhimisho kata ya Kifanya Machi 06,2024,maadhimisho kata ya Luponde Machi 07,2024,kutembelea na kutoa msaada kwa wafungwa gereza la Wilaya ya Njombe pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu Shule ya msingi kibena.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanaambatana na kauli mbiu isemayo "Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe