Wanawake wajasiriamali Halmashauri ya mji njombe wametakiwa kuendelea kushirikiana na kuwezeshana ili kutimiza ndoto zao .
Kauli hiyo imetolewa July 03 ,2023 na Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania(UWT) Ndugu ,Zainab Shomari baada yakukagua mradi wa Uwatikaji wa miche ya parachichi unaofanya na wanawake wa kikundi cha MAWIO kilichopo kata ya Mji Mwema Halmashauri ya Mji Njombe .
Zainabu akiwa ameambatana Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Erasto Mpete pamoja na viongozi wengine kutoka (UWT) taifa na mkoa wa njombe ametoa pongezi kwa wanakikundi hao kwa kazi wanayoifanya ya uwatikaji wa miche ya parachichi kwa pamoja akisema ni wakati sasa kwa wanawake kujiwezesha wenyewe kwa kubuni miradi mbalimbali kwani serikali inatoa mikopo isiyo kuwa na riba ili waweze kujishughulisha na kusaidia kuinua uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Kikundi cha MAWIO ni miongoni mwa vikundi vilivyonufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na serikali kwa vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu.
Kupitia Halmashauri ya Mji Njombe kikundi cha MAWIO kimefanikiwa kupata mkopo kwa awamu mbili ,shilingi milioni 10,000,000/= awamu ya kwanza mwaka 2021 na shilingi milioni 20,000,000/= awamu ya pili mwaka 2022 kikiwa na jumla ya wanawake kumi (10).Aidha kikundi hiki kimefanikiwa katika kazi zake kutoka kufanya uwatikaji wa miche ya parachichi elfu sita(6000) hadi miche elfu kumi na tano (15) mwaka 2022
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe