• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Wataalam World Benki,TAMISEMI watembelea Stendi na Soko Njombe,VAT bado changamoto utekelezaji Miradi

Tarehe iliyowekwa: March 13th, 2020

Timu iliyohusisha Wataalamu kutoka Benki ya Dunia na Ofisi ya Rais TAMISEMI imekagua mwenendo wa shughuli za ujenzi wa Soko na Stendi ikiwa ni hatua za mwishoni kuelekea kumalizika kwa programu hiyo inayofadhiliwa na Benki ya Dunia na kukagua Mapendekezo ya Mradi mpya wa Barabara zinazotarajiwa kuingizwa kwenye Mpango katika Programu zijazo.


Changamoto kubwa iliyobainika katika utekelezaji wa miradi hiyo ikiwa ni kuchelewa kwa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani(VAT Exemption) ambao umesababisha Wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kununua vifaa vya Ujenzi na gharama ya VAT na wakati mwingine kukwama kwa shughuli za ujenzi kutokana na changamoto hiyo.

Akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa utekelezaji wa miradi hiyo Mchumi wa Halmashauri Emma Lunojo amesema kuwa Halmashauri iliamua kufanya utekelezaji wa miradi ya Soko na Stendi kufuatia uchakavu wa miundombinu iliyokuwa ikitumika jambo lililopekea uwepo wa kero kwa watumiaji wakiwemo Wafanyabiashara na Wasafiri.

Aliendelea kusema kuwa kufuatia ujenzi wa miradi hiyo mpaka sasa Wananchi wa Mji wa Njombe wameendelea kunufaika kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza  fursa za ajira, kuongezeka kwa thamani ya ardhi katika maeneo ya mradi  na Halmashauri kuweza kujiongezea mapato kupitia kuongezeka kwa vyanzo vya makusanyo.

 Wakizungumza mara baada ya kutembelea miradi hiyo Timu hiyo ya Wataalamu imesema kuwa licha ya kuwa miradi hiyo inazisaidia Halmashauri kuongeza mapato ni vyema  kuangalia miradi itakayowawezesha Wananchi kuongeza kipato, kuboresha hali ya maisha, kuboresha maeneo ambayo hayajajengwa au kupangwa ili kuweza kuinua hadhi ya maeneo hayo na kupambana na umaskini jambo ambalo limekuwa ni kipaumbele kikubwa  katika utekelezaji wa miradi ya Benki ya Dunia.

Halmashauri ya Mji Njombe ni moja ya Halmashauri 18 zinazotekeleza mradi wa Uboreshaji na  Uimarishaji  Miji (ULGSP) ambapo kwa sasa inatekeleza mradi wa Ujenzi wa Stendi na Soko la Kisasa.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe