Aprili 03 ,2024 timu ya wataalamu kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) pamoja na wataalamu kutoka wizara ya elimu,sayansi na teknolojia imefika mjini Njombe kwa ajili kukusanya taarifa za awali kuhusu athari za kijamii na kimazingira (ESIA) zitakazotokana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kampasi ya chuo kikuu cha Dodoma Njombe.
Timu hiyo imefanya majadiliano na wataalamu katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe ,ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe pamoja na wananchi wa mtaa Kihesa uliopo kata ya Njombe Mjini ambapo mradi huo utatekelezwa.
Mwishoni mwa mwaka 2023 timu ilifika kukagua maeneo yaliyopendekezwa nakuridhishwa na eneo lililopo shule ya sekondari Njombe lenye ukubwa wa hekari 117 pamoja na eneo lililopo Ihahula lenye ukubwa wa hekari 300 litakalotumika kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Mradi wa ujenzi wa kampasi ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Njombe, unatekelezwa chini ya mradi wa elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET). Mradi wa HEET unasimamiwa na wizara ya elimu kwa ufadhili wa Benki ya dunia.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe