Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga amewakumbusha watendaji wa kata na vijiji wajibu walio nao wa kusimamia na kukusanya mapato ya Halmashauri kwenye maeneo yao ya kazi.
Wito huo umetolewa Septemba 22,2023 katika kikao kazi cha Watendaji wa Halmashauri ya Mji Njombe kilichokaa kwa lengo lakukumbusha vyanzo na njia mbalimbali za ukushanyaji mapato pamoja na kujenga uelewa wa mabadiliko yaliyofanywa na serikali kwenye baadhi ya mifumo ya ukusanyaji mapato kwenye Halmashauri.
Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi wa Mji Njombe aliwaomba watendaji hao kwenda kusimamia vema na kwa uadilifu miradi ya serikali ambayo inatekelezwa katika maeneo yao ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kwa ufanisi unaotakiwa,pamoja na kuhakikisha mapato katika maeneo yao yanakusanywa kwa mujibu wa sheria.
Aidha Ndugu Luoga amewaagiza watendaji wa kata na vijiji kwenda kusimamia zoezi la kuandikisha wakulima wapya watakao pata pembejeo za kilimo na kuhuisha taarifa zao kwa wale waliokuwa wamejaza awali.
Naye Benjamini Sibanulo Kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Njombe akizungumza katika kikao kazi hicho amesema serikali haita vumilia endapo Kuna mtendaji atabainika kujihusisha na vitendo vya rushwa
Kikao hicho kiliwakutanisha watendaji pamoja na wakuu wa idara zenye vyanzo vya ukusanyaji wa mapato ndani ya Halmashauri ya Mji Njombe.
Ni muda sasa wa kwenda kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili tuweze kuyafikia malengo ya Mhe Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe