Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Njombe Mjini, Samson Medda, amewahimiza waandikishaji ngazi ya kata kusimamia kwa umakini zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika maeneo yao.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya uandikishaji yaliyofanyika Tarehe 05,Januari 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe Njombe, Medda aliwataka watendaji hao kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia maelekezo ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC). Alisisitiza kuwa uangalifu na uzingatiaji wa maelekezo ni muhimu ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kama lilivyokusudiwa.
"Ni muhimu kutumia vifaa vya uandikishaji kwa uangalifu na kuzingatia maelekezo yote ya tume ili kuepusha changamoto zisizotarajiwa na kuhakikisha kazi inafanyika kwa usahihi," alieleza Medda.
Mafunzo hayo yalijikita kuelekeza namna ya ujazaji wa fomu kwa kutumia mfumo wa uandikishaji wa wapiga kura pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya uandikishaji, hususan vifaa vya bayometriki,lengo ikiwa ni kuwapa maarifa ya kuwafundisha waendeshaji wa vifaa hivyo na waandishi wasaidizi watakaofanya kazi katika zoezi hilo.
"Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora."
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe