Pamoja na mafanikio kwenye kadi alama katika utekelezaji wa Viashiria vya Mkataba wa Lishe kipindi cha robo ya nne Aprili- Juni mwaka fedha 2023/2024, Halmashauri ya Mji Njombe kwa kushirikiana na wadau na vituo vya kutolea huduma za afya ,imefanya jitihada kwa kuhakikisha, Watoto wanaohudhuria kliniki wameweza kurudishwa kwenye Tarehe zao za kuzaliwa,hii itasadia ufuatiliaji wa karibu wa hali ya ukuaji wa mtoto pamoja na upimaji wa hali zao lishe.
Mama mjamzito anapaswa kuhudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito ,kula lishe bora,kupata muda wakupumzika ,kutumia dawa za minyoo ,dawa za kumkinga na malaria ,dawa za kuongeza madini na damu.
Baada yakujifungua mama anatakiwa kupumzika ,kula vyakula vitakavyomuwezesha kupata maziwa yakutosha na kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita pamoja na kuhakikisha mtoto anapelekwa kliniki nakupatiwa chanjo zote ili kumkinga na hatari yakupata magonjwa au ulemavu wa kudumu.
Kumbuka "Lishe ya Mwanao ni Mafanikio Yake,kujaza tumbo siyo Lishe Jali unachokula na unachomlisha mwanao"
Njombe bila udumavu inawezekana.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe