Wazazi na walezi mkoani Njombe wametakiwa kutoa kipaumbele kwenye suala la lishe bora ili kuondokana na udumavu.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. David Ntaindwa aliyemwakilisha Mganga Mkuu Mkoa wa Njombe katika maadhimisho Siku ya Afya na Lishe yaliyofanyika June 12,2023 Kata ya Ramadhani iliyopo Halmashauri ya Mji Njombe.
Dkt Ntaindwa amewasihi wazazi na walezi kuhakikisha wanazingatia makundi yote ya vyakula bora kwa watoto ili kuepukana na changamoto ya udumavu.
"Siku hii ya Afya na Lishe inatukumbusha wajibu wetu kama wazazi na walezi kuzingatia afya zetu na matumizi ya lishe bora kwa watoto, tunaamini elimu ya lishe ambayo imetolewa na wataalamu wa afya itaenda kuwasaidia katika kuanda vyakula bora kwa watoto wetu ili tuepukane na udumavu katika mkoa wetu"
Kwa upande wake Diwani Kata ya Ramadhani Mhe.Nickson Nganyage amewatahadharisha wazazi kutotumia muda mwingi katika shughuli binafsi za kijamii na kiuchumi baadala yake wajikite katika malezi ya watoto ili kupunguza changamotoya udumavu katika mkoa wa njombe .
Aidha Afisa Lishe Mkoa Njombe Betha Nyigu amewaomba wazazi kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya wataalamu wa afya na kuhakikisha wanawapa watoto kipaumbele kama wanavyo tumia muda mwingi katika kazi zao.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe