Mafunzo yaliyowahusisha watumishi wa umma katika Halmashauri ya Mji Njombe yaliyofanywa na Wataalamu kutoka Benki Kuu ya Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini yakiwa na lengo la kutoa elimu juu ya utambuzi wa noti bandia na utunzaji bora wa fedha.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Meneja wa Operesheni kutoka Benki hiyo Melchiades Rutayebesibwa amesema kuwa kumekuwa na wimbi la watu wasiokuwa na nia njema ambao wanaingiza pesa bandia kwenye mzunguko wa kifedha na hivyo kupelekea hujuma kwenye uchumi wa Nchi.
Kwa upande wake Petty Ndowo ambaye ni Mtaalamu kutoka Benki ya Tanzania amewataka Watumishi kuendelea kuwa mabalozi wazuri na kuelimisha jamii juu ya utunzaji bora wa fedha.
“Jamii inapaswa kutambua juu ya utunzaji wa fedha kwani fedha hizi ni kodi za Wananchi.Utengenezaji wa fedha unagharimu pesa nyingi. Fedha ambazo pengine zingeweza kutumika kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo” Alisema Petty
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga amesema kuwa elimu hiyo ni muhimu kwa Watumishi na amewataka Watumishi wa umma kuhakikisha kuwa wanatumia mnyororo ulio sahihi wa kujipatia fedha ikiwa ni kufanya kazi kwa bidii na kuhakisha kuwa wanatumia muda wao wa ziada kushiriki katika shughuli za ujasiriamali ikiwa ni sambamba na kulima na kufuga ili kuweka kujiongezea fedha katika njia za uhalali.
Miongoni mwa majukumu muhimu ya Benki Kuu ya Tanzania ni kutengeneza pesa, kusambaza pesa na kuondoa pesa zilizoisha kwenye mzunguko.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe