Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Twilumba Mwalongo, amewataka watumishi wa Kitengo cha Ardhi katika Halmashauri ya Mji Njombe kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi.
Akizungumza na watumishi hao Tarehe 17 Desemba 2024 katika kakao cha kitengo hicho, alisema ni muhimu kila mtumishi kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma na kuepuka vitendo vya rushwa kazini.
Alihimiza uzalendo , umoja, mshikamano na kuhakikisha wanashirikiana vyema katika utekelezaji wa majukumu yao kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi.
Alisisitiza kuwa nidhamu na uwajibikaji ni nguzo muhimu za utumishi bora wa umma.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe