• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

WATUMISHI WA DINI WATOA DUA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

Tarehe iliyowekwa: May 31st, 2025

Mei 30, 2025 Watumishi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali, wakiongozwa na Mchungaji Nelson Godiwe, wameungana kwa pamoja katika ibada maalum ya kuwaombea watumishi wa Halmashauri ya Mji Njombe.

Ibada hiyo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe, ikiwa na lengo la kuwaombea watumishi hao amani, mshikamano, upendo, umoja na mafanikio katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mchungaji Nelson Godiwe kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) alisema kuwa sala na dua ni nguzo muhimu katika kuhakikisha mazingira ya kazi yanabaki kuwa ya utulivu na yenye maadili ambapo  alisisitiza kuwa viongozi wa umma wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuomba baraka za Mungu kwa ajili ya kazi zao.


“Watumishi wa serikali ni mihimili muhimu ya maendeleo ya taifa, maombi haya ni muhimu ili kuwajengea msingi wa maadili, upendo na uaminifu katika utendaji wenu  wa kila siku,” alisema Mchungaji Godiwe.

Kwa upande wake, Shehe Rajabu Msigwa alieleza kuwa mafanikio ya taifa lolote yanatokana na mshikamano na upendo miongoni mwa wananchi wake ambapo  ushirikiano kati ya viongozi wa serikali na wananchi unapaswa kuimarishwa kupitia misingi ya heshima na maadili ya kidini.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Bi. Kuruthum Sadick katika salamu zake kwa washiriki wa ibada hiyo, alikumbusha kuwa uzima na mafanikio hutoka kwa Mungu ambapo alisema kuwa ni wajibu wa kila mtumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na moyo wa kujitolea, kwa kuwa wanahudumia wananchi na taifa kwa ujumla.

Ibada hiyo imeonyesha mshikamano wa kiroho kati ya viongozi wa dini na watumishi wa serikali, ikiwa ni hatua ya kuimarisha maadili na kuongeza moyo wa uzalendo na uwajibikaji katika utumishi wa umma.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Halmashauri ya Mji Njombe yazindua wiki ya Mazingira kwa kufanya Usafi Idundilanga

    May 31, 2025
  • WATUMISHI WA DINI WATOA DUA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

    May 31, 2025
  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe