Watumishi wa afya kutoka vituo 42 vya afya katika Halmashauri ya Mji wa Njombe wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa GoTHoMIS, ambao unahusika na usimamizi wa shughuli za uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya.
Mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku 2 yanalenga kuwawezesha watumishi hao kuweza kutumia mfumo huo kwa ufanisi ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. Mbali na mafunzo, watumishi hao pia wamepatiwa vishikwambi (tablets) vitakavyowasaidia kuratibu na kusimamia shughuli za mfumo huo kwa urahisi zaidi.
Mfumo wa GoTHoMIS umeundwa ili kuhakikisha taarifa za wagonjwa, dawa, na malipo zinahifadhiwa kwa usalama na kupatikana kwa haraka, hivyo kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya.
Mafunzo haya ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha matumizi ya mifumo ya kidijitali yanaboreshwa katika sekta ya afya, kwa lengo la kuongeza uwazi, kupunguza upotevu wa rasilimali, na kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe