Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka Mei 14,2024, ametoa rai kwa watumishi wa Serikali kufanya uwekezaji kwenye shughuli mbalimbali ili kujiongezea kipato.
Ametoa rai hiyo alipo mtembelea mwekezaji Ibrahim Mkinga anayejenga nyumba ya kulala wageni katika kijiji cha Mavanga kilichopo Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe.
" Nilipoona kwenye ratiba ya mwenge kuna mradi wa wananchi nikawaambia watumishi wenzangu wa Serikali tuje tutembelee ili tuweze kujifunza kwa sababu una miaka 49,una lima, una watoto wanne, unafanya biashara yako ya makorokoro kidogo lakini umekuwa mtu mwenye mafanikio makubwa, tunakupongeza Sana kwa jitihada zakuinua uchumi"
Kwa upande wake mwekezaji Ibrahim Mkinga ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mbolea ya ruzuku.
"Bila ruzuku wengi tusingeweza kwa msimu uliopita nimepata mavuno mengi gunia 350 kwa ekari 35 kabla ya ruzuku haikuwa hivyo" Alisema Bwn. Mkinga.
Aidha Bwana Ibrahim alitoa ushauri kwenye matumizi mazuri ya fedha kwa maendeleo.
"Tunapopata fedha tuitunze na tuwekeze kwenye vitu vya msingi, mradi huu utanisaidia mimi mwenyewe, watoto wangu na kizazi kijacho." Alisema
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe