Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe Erasto Mpete amewaomba wauzaji wa dawa za mifugo kununua dawa na chanjo kutoka kwenye vituo na mamlaka zilizo thibitishwa na serikali.
Septemba 06 ,2023 Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kanda ya nyanda za juu kusini kituo cha Iringa ilifanya mafunzo maalumu kwa wataalamu , wafugaji ,wamiliki wa maduka na wauzaji wa madawa ya mifugo yaliyolenga kutoa elimu ya chanjo na uchanjaji pamoja na matumizi sahihi ya dawa za mifugo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe. Erasto Mpete alitoa shukrani kwa wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa kuwezesha elimu hiyo ya matumizi sahihi ya chanjo na dawa za mifugo kwa wafugaji ,wataalamu wa mifugo pamoja na wauzaji wa dawa za mifigo waliopo Halmashauri ya Mji Njombe.
Aidha ametumia fursa hiyo kushauri wauzaji wa dawa za mifugo mjini Njombe kuwa na umoja ambao utawasaidia kupeana elimu na taarifa mbalimbali kuhusiana na masuala ya chanjo na dawa za mifugo.
Mafunzo hayo yalitoa elimu kwa wafugaji kuweza kufahamu na kutofautisha kati ya chanjo na dawa ,namna sahihi ya utunzaji wa chanjo za mifugo,namna yakutambua chanjo feki zinazozalishwa hapa nchini,namna sahihi ya uchanjaji na anayestahili kutoa chanjo pamoja na utunzaji na usafi wa mabanda ya mifugo ili kuzuia magonjwa.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe