Mkufunzi wa sayansi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ngazi ya Taifa, Martini Chuwa, amewataka wazazi na walezi Mkoa Njombe kuhakikisha watoto wanapata malezi bora, lishe sahihi, na vichezeo (vichangamgamshi) vinavyowasaidia kielimu na kihisia.
Akizungumza Agosti 18,2025 na wakazi wa Soko Kuu Njombe, Chuwa alisema kuwa malezi bora hayahusishi tu huduma za msingi kama chakula, malazi, afya na usalama, bali pia upendo, mwongozo wa maadili, nidhamu chanya, na msaada wa kihisia unaomjenga mtoto kimaadili na kisaikolojia akiwa katika makuzi.
Akiendelea kuzungumza na wananchi wa Soko kuu Njombe Chuwa alisisitiza umuhimu wa wanaume kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wao badala ya kuachia jukumu hilo kwa wanawake pekee.
“Malezi bora lazima yawe ya kisayansi na yenye kuzingatia hatua za ukuaji wa mtoto, wanaume msiwaachie wanawake kwasababu watoto wanahitaji malezi yapande zote mbili ,mtoto wakike atatamani kuishi vizuri na mwanaume kupitia baba yake na mtoto wakike atataka kujifunza kuishi vizuri na mke wake kupitia mama yake anavoishi jambo ambalo litawasaidia wakiwa wakubwa kumjuwa mke bora ni yupi na mwanume bora ni yupi” aliongeza Chuwa.
Kwa upande wake, Afisa Lishe wa Mkoa wa Njombe, Bi. Bertha Nyigu, kupitia Mradi wa Lishe ya Mwanao unaosimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Njombe na kudhaminiwa na UNICEF, aliwataka wazazi hususani wale wanaoshinda sokoni kuhakikisha wanawapeleka watoto wao katika Kituo cha Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Watoto kilichopo Soko Kuu Njombe kwa lengo la kupunguza changamoto ya udumavu miongoni mwa watoto ambayo bado ipo katika mkoani Njombe.
Ni jukumu la kila mlezi kuhakikisha watoto wanapata malezi bora, lishe yenye afya, na mafunzo ya maadili mema na malezi bora yatakayosaidia mtoto kukua akiwa na nidhamu, upendo, na mwongozo wa maadili, na lishe sahihi itakayomsaidia kupata afya njema na ukuaji wa kisaikolojia jamba ambalo litasaidai kuwaandaa watoto kuwa raia wenye uwezo wa kuchangia maendeleo ya familia, jamii, na taifa kwa ujumla.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe