Katibu tawala Mkoa wa Njombe Bi.Judica Omary ametoa rai kwa wazazi ,walezi na jamii kwa ujumla kuhamasishana ili walengwa wa chanjo ya saratani ya malango wa kizazi ambao ni mabinti wenye umri kuanzia miaka 9 hadi 14 waweze kufikiwa.
Bi.Judica ametoa rai hiyo Aprili 23,2024, katika kituo cha afya Uwemba wakati wa ufunguzi wa kampeni ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV)
"Mtoto asiyepata Chanjo ni hatari kwa maisha yake na kwa jamii inayomzunguka kwani anaweza kuambukizwa au kuwaambukiza wengine ,hivyo ndugu wananchi ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anakuwa mlinzi wa mwenzake" alisema Bi. Judica Omary.
Aidha amesema kuwa Mkoa wa Njombe unatarajia kutoa chanjo hiyo kwa asilimia 80 ya walengwa wa chanjo hiyo.
"Madhumuni ya wiki hii ni kutoa dozi ya chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa kiwango cha asilimia 80 kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 ,niwaombe wazazi na walezi tujitokeze na kuhakikisha mabinti zetu wanapata chanjo hii ".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe