Wazazi na walezi Wilaya ya Njombe wamehimizwa kuwapeleka Watoto kupatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua ambao umeonekana ni changamoto kwa Mkoa wa Njombe .
Wito huo umetolewa Februari 13,2024 na Katibu Tawala Wilaya Njombe Bi .Agatha Mhaiki akiwa katika Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Surua Rubella kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe ambapo Katibu Tawala Wilaya ya Njombe amewataka wazazi wenye watoto wote wenye umri kuanzia miezi 9 hadi miezi 59 (chini ya miaka 5) kupewa chanjo hiyo ili kuweza kuongeza kinga kwa watoto pamoja na kuzuia kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.
Aidha amewaomba wazazi na walezi wajitokeze wafike vituo vyote vinavyotoa huduma za afya ya mama na mtoto zikiwemo hospitali,vituo vya afya, zahanati na sehemu zitakazopangwa ikiwemo huduma tembezi na huduma za mkoba hususani mashuleni na vituo vya kulelea Watoto wadogo .
Kwa upande wake Filoteus Mligo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri amewaombwa wataalamu kutoa elimu kwa wananchi juu ya hatari ya ugonjwa wa surua pamoja na kuhimiza juu ya umhimu wa kupatiwa chanjo hiyo.
Kaulimbiu ya mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Surua inasema “Onyesha Upendo, Mpeleke Mtoto Akapate Chanjo”.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe