Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe, Mhe. Erasto Mpete, ametoa wito kwa wazazi wote wa Halmashauri ya Mji Njombe kuwapa uhuru na utulivu watoto wa darasa la saba watakaofanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi tarehe 11 na 12 Septemba, 2024 nchini kote.
Akizungumza Tarehe 09 Septemba, 2024, wakati wa ziara yake katika shule za Msingi Kata ya Utalingolo, pamoja na Shule ya Msingi Ihanga na Chilima, iliyolenga kuwatakia kheri wanafunzi wote wa Darasa la Saba katika mtihani wao wa Taifa,Mhe. Mpete amesisitiza umuhimu wa watoto kupumzika wanapokuwa nyumbani ili wawe na utulivu wa akili wanapofanya mitihani yao.
Pia, Mhe. Mpete amewashauri wazazi kuhakikisha watoto wanapewa chakula bora na rafiki kwa afya zao, ambacho hakitasababisha matatizo wakati wa mitihani, ili kuepusha changamoto zinazoweza kuathiri utulivu ndani ya chumba cha mtihani.
Jumla ya wanafunzi 3,770 wanatarajiwa kufanya mtihani huu wa taifa, ambapo wavulana ni 1,737 na wasichana ni 2,033.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe