Jamii Mjini Njombe imetakiwa kutilia mkazo katika maadili na malezi kwa watoto watakao lijenga taifa imara siku za mbeleni.
Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage Ndugu Francis Msanga katika mkutano wa robo ya mwaka wa mapato na matumizi pamoja na kujadili shughuli mbalimbali za maendeleo ya mtaa huo .
Katika mkutano huo Bwana Francis Msanga Mwenyekiti wa Mataa amewaomba wananchi wa mtaa huo kuhakikisha wanawatunza watoto vizuri ili kuepukana na watoto wanaopotea mitaani jambo ambalo linatia mashaka katika malezi ya watoto.
"Ndugu zangu wananchi watoto hawa tumewazaa sisi kwanini tuwa kimbie kulea,utakuta mama au baba akitoka asubuhi anawaza tu kazi zake anamsahamu hata mtoto wake anaendeleaje na anashinda na watu gani niwaombe sanaa wananchi ni muda sasa wa kupunguza starehe na tujikite katika malezi wa watoto tulio wazaa" Alisema Mwenyekiti wa Mtaa Kambarage Francis Msanga.
Kwa upande wake Nicodemass Phuni Mtendaji wa Mtaa wa Kambarage amewaomba wananchi wote kujitoa katika kuchangia ujenzi wa zahanati ya Mtaa wa Kambarage ambayo kwa jitihada za wananchi tayati hatua za awali zimeanza kufanyika ambazo ni kusogeza mawe ,mchanga pamoja na kuchangia ujenzi wa shule ya Msingi Igeleke ujenzi ambao tayari umeanza kwa hatua za wali za kuchimba msingi , kung'oa visiki na kusogeza mawe .
Akiendelea kuzungunza na wananchi mtendaji wa mtaa ametoa shukrani za dhati kwa Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Mhe .Deo Mwanyika Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, kampuni ya Mpete Agrovet ,Wananchi na Wadau wote walio wiwa kuchangia michango yao ujenzi wa zahanati na Shule ya Msingi Igeleke kitu ambacho kitainua taalumua ya watoto na kuimarisha afya za wananchi mara baada ya kukamilika kwa miradi hiyo.
Naye Frorida Kiecha Polisi kata ya Njombe Mjini amewaomba wazazi na walezi katika kuelekea sherehe za kufunga mwaka kuwa makini na mienendo ya watoto ili wasiende katika kumbi za starehe pamoja na kukemea vitendo viovu vinavyo tokea katika jamii .
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe