Wazee wa Kijiji cha Lwangu kilichopo kata ya Kifanya, Halmashauri ya Mji Njombe, wametakiwa kutoa taarifa za ukatili mara zinapotokea ili kuepukana na madhara makubwa yanayotokana na ukatili wa kijinsia kwenye jamii.
Rai hiyo imetolewa Machi 27,2024 na Bwana Gracian Panza mwezeshaji wa TASAF Kijiji cha Lwangu wakati akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanufaikawa wa mpango wa kinusuru kaya masikini hususani wazee ambao wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali za ukatili katika jamii haswa wakiwa majumbani na kwenye familia zao
Panza amesema wazee wakinyimwa haki zao za msingi ,kukosa mahitaji mhimu ya binadamu ,kunyimwa fursa za maendeleo , kufanyiwa vitendo vya ukatili kama kubakwa na kulawitiwa na wengine kukosa haki ya kuishi kutokana na imani potofu za kishirikina kwa wazee.
Kwa upande wake Renatusi Masasi Mwenyekiti wa Kijiji hicho amewaombwa wanufaika wa TASAF kuhakikisha wanajiunga na vikundi mbalimbali vya kiujasiriamali ili kuweza kujipatia kipato badala yakutegemea fedha za TASAF pekee kujiendeleza.
Aidha warsha hiyo ilitoa fursa yakuchagua uongozi wa wazee wa kijiji cha Lwangu kwa ajili ya kusikiliza kero na kutatua changamoto ambazo wazee wamekuwa wakizipata kwenye jamii na maeneo wanayaishi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe