Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemaliza mgogoro wa muda mrefu baina ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini Njombe na Wananchi wa kijiji cha Magoda mtaa wa Lunyanywi katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Uamuzi huo unafuatia maridhiano yaliyofikiwa baina ya pande zote mbili za mgogoro baada ya timu iliyoundwa ikihusisha wawakilishi kutoka kwa wadai na wale wa KKKT, wataalamu wa ofisi ya ardhi mkoa na halmashauri, TAKUKURU, Polisi na ofisi ya usalama mkoa kuwasilisha ripoti yake.
Akihitimisha mgogoro huo kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji Njombe Agosti 9, 2023, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema, ili kumaliza mgogoro huo ni vyema wananchi wanaodai kupokea viwanja 400 kama kifuta jasho pamoja na urasimishaji wa makazi kwa wale walioingia kwenye eneo lenye mgogoro bila kufuata taratibu.
Aidha Waziri wa Ardhi amelitaka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini Njombe kuhakikisha linalinda maeneo yake.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe