Kuelekea Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Mji Njombe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi Kuruthum Sadick, anapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa, kuanzia Tarehe 10 hadi 17 Juni, 2024 itakuwa ni wiki maalumu ya huduma kwa wananchi wote wanapatiwa huduma katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Huduma zitakazotolewa ni pamoja kushughulikia malalamiko, utatuzi wa kero na migogoro, utoaji wa Hati na umilikishwaji wa ardhi, kulipia kodi ya pango la ardhi, kulipia vibali vya ujenzi, kulipia leseni za biashara na vileo, upimaji wa afya bure na ushauri, uchangiaji wa damu, elimu ya lishe, uandikishaji wa vitambulisho vya wajasiriamali pamoja na huduma nyingine.
Wananchi wote mnakaribishwa.
Huduma bora ni kipaumbele chetu.
Tunawajadili na tunakuthamini.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe