Halmashauri ya Mji Njombe inatekeleza zoezi la huduma kwa wateja katika eneo la Kituo cha Mabasi (Stendi ya Zamani) Njombe Mjini, kuanzia tarehe 01/09/2025 hadi 04/09/2025.
Lengo la zoezi hili ni kusogeza huduma karibu na wananchi, kutatua changamoto mbalimbali, na kupunguza adha ya wananchi wanaolazimika kufuata huduma hizo makao makuu ya Halmashauri yaliyopo Lunyanywi.
Huduma zitakazotolewa ni pamoja na:
•Usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa
•Huduma za leseni za biashara
•Kliniki ya ardhi
•Huduma za msaada wa kisheria
•Huduma za kilimo, mifugo na misitu
•Huduma za afya na mazingira
•Kupokea na kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi
Aidha, kutatolewa taarifa muhimu kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, pamoja na mwongozo wa namna ya kuwasilisha maombi ya mikopo hiyo.
Wananchi na wadau wote wa Halmashauri ya Mji Njombe mnakaribishwa kushiriki na kupata huduma hizi muhimu.
Huduma zote zitakuwa bure, bila malipo yoyote.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe