Ni katika ziara ya siku moja yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, ambapo Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole amesema kuwa Wilaya ya Njombe imeweza kuendelea kutekeleza miradi mizuri yenye ubora na itakayolenga kutatua kero kwa Wananchi.
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi inayotekelezwa kwa fedha za mapambano ya Uviko na miradi inayojengwa kupitia nguvu za wananchi na Mapato ya ndani ya Halmashauri kikiwemo Kituo cha Afya Mjimwema na Ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa shule ya sekonari mpechi Ngole amesema kuwa Serikali imeendelea kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa maendeleo ya wanawafikia wananchi.
“Niwapongeze Wananchi wa Kata ya Mjimwema kwa kuamua kuanza ujenzi wa kituo cha afya. Kituo hiki kitasaidia kutatua changamoto ya kituo kilichopo eneo la mjini ambacho kinahudumia Wananchi wengi. Kata ya Mjimwema ni Kata ya kimkakati ndipo yalipo Makao makuu ya mkoa na ndipo eneo ambalo mji unapokua.Kkituo hiki kitakua na msaada mkubwa kwani Taasisi nyingi za Kiserikali zitakapokuwa. Niombe Mkurugenzi kuhakikisha kuwa unatoa kipaumbele kupitia mapato ya Halmashauri kuhakikisha kuwa ujenzi wa Kituo hiki unaendelea ili uweze kukamilika na wananchi kupata huduma.
Katika Shule ya Sekondari Mpechi shule iliyonufaika na ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa vyenye thamani ya shilingi milioni 100 mradi unaotekelezwa kupitia fedha za mapambano ya UVIKO mwenezi wa Mkoa wa Njombe amesema kuwa anashangazwa na baadhi ya Wananchi wanaopinga jitihada za Rais katika kuletea maendeleao kwa kuboresha mahusiaono na Mataifa mbalimbali na amesema kuwa tabia hiyo inapaswa kukemewa vikali
“Ndugu zangu katika kipindi kama hiki miaka iliyopita wazazi walikua hawakai majumbani,ni muda ambao watu walikua wanajificha kukimbia michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya kupokea kidato cha kwanza. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika Serikali inajenga vyumba vya madarasa kila sehemu kwa ajili ya kidato cha kwanza. Hatuna budi kupongeza na kuishukuru Serikali kwani tungekuwa tunachangishwa muda huu lakini sasa tunajengewa vyumba vya madarasa.”Alisema
“Ilani ya chama cha mapinduzi imeweka bayana kuwa itaendelea kuboresha na kudumisha mahusiano na mataifa mengine ili kufungua uchumi na kuwafuata wengine. Mheshimiwa Rais anatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi na ndio maana leo tunanufaika na miradi lakini kila siku tumekuwa tukipata wawekezaji katika sekta mbalimbali jambo litakalosaidia kuchochea uchumi na kuongeza ajira kwa vijana wetu”Alisema Ngole
Aidha wajumbe hao walishauri miradi ya UVIKO inayotakiwa kukamilika kufikia desemba 15 2021 kuhakikisha kuwa inakamilishwa na kuzingatia ubora uliokusudiwa bila kulipua.
Katika kuunga mkono jitihada za Wananchi katika maeneo inapotekelzwa miradi ya maendeleo Ngole ameahidi kutoa mifuko 250 ya Saruji na miche 300 ya parachichi kwenye maeneo yaliyopitiwa na Wajumbe hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa kuunga mkono kufanikisha utekelzaji wa miradi hiyo na ameahidi kuendelea kusimamia utekelzaji wa ilani katika wilaya na kuhakikisha kuwa miradi inakuwa bora na yenye tija kwa jamii.
Ziara hiyo iliyogawanyika katika makundi manne iliweza kuzifikia Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe Ikiwemo Ludewa,Makete,Wang'ing'ombe na Wilaya ya Njombe ambayo imeundwa na Halmashauri tatu ikiwemo Halmashauri ya Mji Makambako,Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe