Diwani wa Kata ya Uwemba Mhe. Jactani Mtewele amewaombwa wananchi wa kijiji cha Makanjaula na Njomlole kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita ambayo inafanya kazi kubwa kwenye maendeleo.
Amezungumza hayo Mei 16 ,2024 na wananchi hao nakutoa rai kwao kuendelea kuiamini Serikali ambayo inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika vijiji hivyo.
"Kwa kipindi cha miaka mitatu Serikali imetekeleza miradi ya ujenzi wa Madarasa,Zahanati ,Ukarabati wa Miundombinu ya Barabara katika vijiji vyetu, huduma ya nishati ya umeme kwa mara ya kwanza katika kijiji cha Makanjaula ,upatikanaji wa maji kwa wakati sambamba na mikopo nafuu ya pembejeo za kilimo kwa wakulima wa zao la viazi na Parachichi tuendelee kuiamini Serikali inatujali".Alisema.
Naye Mtendaji wa kata hiyo, Christina Njogela amewataka wananchi kulinda amani katika maeneo yao huku akiwaasa vijana kuacha tabia bwete ambayo inapelekea vijana kujiunga na makundi ujambazi.
Kwa Upande wake Diwani wa Viti Maalumu Mariamu Chundu amewataka wanawake wa maeneo hayo kuhakikisha wanazingatia malezi kwa watoto pamoja na kuzingatia elimu ya lishe ambayo inatolewa na wataalamu kutokana na hali ya kuongeza kwa tatizo la udumavu kwa Mkoa Njombe .
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe