• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Zahanati mpya Luponde yaanza kutoa huduma.Wananchi wasema ujenzi kituo cha afya Luponde kazi iendelee

Tarehe iliyowekwa: April 26th, 2021

Wananchi wa Kijiji Cha Luponde Kata ya Luponde Halmashauri ya Mji Njombe wamefurahishwa na uzinduzi wa zahanati mpya ya Luponde katika Kijiji hicho ambapo kwa takribani miaka 45 kijiji hicho kukosa Zahanati na kupelekea Wananchi kutibiwa katika zahanati za mbali na zahanati ya kiwanda Cha chai luponde jambo lililokuwa likisababisha kero kwa wananchi  kutokana idadi kubwa ya wagonjwa na hivyo  kupelekea kuzidiwa kwa zahanati ya kiwanda.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa Zahanati hiyo Afisa Mtendaji wa Kijiji cha  Luponde Lucy Kayombo amesema kuwa uzinduzi wa huduma katika Zahanati hiyo mpya ni mkombozi kwa Wananchi wa Kata hiyo na maeneo ya jirani kwani kwa muda mrefu Kijiji hicho hakikuwahi kuwa na zahanati ya Serikali jambo lililowasukuma wananchi hao kuanza ujenzi na wameishukuru Halmashauri kwa kuchangia ujenzi na kuwapatia vifaa tiba, samani, mganga na mhudumu wa Afya kwa ajili ya kuendesha Zahanati hiyo.

"Ujenzi wa Zahanati hii umegarimu kiasi Cha shilingi milioni themanini na tisa laki saba na elfu kumi hii ikiwa ni mchango wa Halmashauri,nguvu za Wananchi, fedha za wahisani na mfuko wa jimbo ambapo Zahanati hii itahudumia Wananchi zaidi ya elfu nne.”Alisema

 

Diwani wa Kata ya Luponde Ultrick Msemwa amesema kuwa anawashukuru Wananchi wa Kata hiyo kwa ushiriki wao katika kuchangia miradi ya maendeleo na kuwaomba kutoa ushirikiano wa dhati ili kufanikisha ujenzi wa kituo cha afya ambapo kwa sasa wameshaanza ujenzi wa Msingi kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

"Leo nitatoa mchango wa shilingi laki tano kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa kituo Cha Afya Luponde ambapo tunataraji huduma zitakuwa bora zaidi. Mpango wetu ni kuwa ndani ya miaka miwili tunakamilisha ujenzi wa majengo yote muhimu ya kituo Cha Afya ili tuweze kwenda kwenye utekelezaji wa miradi mipya" Alisema Msemwa Diwani wa Kata hiyo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amesema kuwa Wananchi wa Kijiji cha Luponde hawana budi kujipongeza kwa hatua hiyo kwani Zahanati hiyo ni miongoni mwa zahanati bora na kuahidi kushirikiana nao kwenye ujenzi wa kituo cha afya.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Romanus Mayemba   amewapongeza Wananchi wa Kata hiyo kwa hatua hiyo na amewataka Wananchi hao kuwa mstari wa mbele na kujitoa ili kituo Cha Afya kiweze kujengwa na kukamilika. Aidha amewataka Wananchi hao kujiandikisha na huduma ya bima ya afya CHF iliyoboreshwa ili, zahanati hiyo iweze kujiendesha kwa kuwa na upatikanaji wa dawa za uhakika na zakutosha kwa kipindi Cha mwaka mzima.

“Zoezi la ujenzi wa kituo Cha Afya unakwenda kuanza mara moja. Lakini Halmashauri haitafanya chochote kama Wananchi hamtaanza ujenzi.Tunatarajia kuwapatia mifuko 250 ya saruji kadri mlivyoomba  lakini hatutaki iwe stoo tuanze ujenzi kwa kile ambacho mtakua mmechangia."Alisema mayemba

Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti baadhi ya Wananchi wa Kata ya Luponde wamepongeza uzinduzi wa Zahanati hiyo na kuahidi kushiriki kwenye uanzishaji wa ujenzi wa kituo Cha Afya

Roida malumbo, Marsela Ngailo na Oben Mkolwe wakazi wa kijiji Cha luponde wanasema kuwa uzinduzi wa Zahanati hiyo ni hatua muhimu kwao na wamehamasika kuanza uchangiaji wa kituo Cha Afya

 "Changamoto kubwa tuliyokuwa nayo ni ukosefu wa huduma.Ukipata mgonjwa usiku inabidi usafiri mbali kwenda kupata huduma huku barabara ikiwa si rafiki.Tunaomba Wananchi tuchangie kwa bidii ujenzi wa kituo Cha Afya ili tuweze kupata huduma za upasuaji na huduma nyingine ziweze kuwa hapa.Alisema

Uzinduzi wa Zahanati ya Luponde unaifanya Halmashauri ya Mji Njombe kuwa na jumla ya Zahanati 52 na kuanza kwa ujenzi wa kituo Cha Afya Luponde kufanya ongezeko la vituo vya Afya 4 ambapo kwa sasa ipo katika ukamilishaji wa kituo Cha Afya makowo na kifanya vyote vikijengwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri na nguvu za Wananchi.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe