Tarehe 08 Juni 2025, ndoto za kuwa na zahanati ya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa kijiji cha Mamongolo kilichopo kata ya Makowo, Halmashauri ya Mji Njombe imetimia baada zahanati mpya yenye thamani ya zaidi ya milioni 146 kuzinduliwa.
Zahanati hiyo imezinduliwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Dkt.Jabil Juma kwa niaba ya Mkurugenzi,ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa eneo hilo.
Kwa miaka mingi wananchi wa kijiji cha Mamongolo walikuwa wakitumia jengo la zamani lisilokidhi mahitaji, lakini sasa zahanati mpya imezinduliwa yenye Chumba cha kisasa cha kujifungua kilichounganishwa na chumba kupumzika mama na mtoto baada kujifungua,Sehemu ya kutolea huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) iliyoboreshwa,Maabara ya kisasa,Chumba cha kulaza wagonjwa wanaohitaji huduma kwa saa 24 naStoo ya dawa yenye sehemu ya kutolea dawa.
Tayari vifaa tiba vyenye thamani ya TSh Milioni 33 kwa ajili ya kuanza kazi rasmi vipo katika zahanati ya Mamongolo.
Zahanati hii mpya imegharimu jumla ya TSh Milioni 146.24, zinazojumuisha fedha kutoka Serikali kuu,michango ya wananchi,mapato ya ndani ya kijiji na fedha za mapato ya ndani ya Halmashuauri.
Halmashauri ya Mji Njombe inatoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuimarisha afya ya jamii.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe