Mkulima wa Zao la Parachichi Kutoka Halmashauri ya Mji Njombe Ndg Frank Msuya ameshika nafasi ya kwanza Kitaifa kama mkulima bora wa zao la parachichi kwenye maonesho ya Kimataifa Nanenane mwaka 2023.
Ndg Frank Msuya ni miongoni wanakikundi cha KIWAWANJO anayemiliki shamba la parachichi lenye ukubwa wa ekari 156 likiwa na idadi ya miti ya parachichi 10,000.
Mkulima Frank Msuya Agosti 10,2023 amekabidhiwa zawadi yenye thamani ya shilingi milioni 10.5 ambayo ni Power Tiller kwa ajili yakufanyia shughuli za kilimo.
Mkulima huyu amefanikiwa kuwa miongoni mwa wakulima wanaozalisha parachichi zenye ubora zinazoanza kuuzwa kuanzia mwezi Agost.
Aidha, Halmashauri ya Mji Njombe inatoa pongezi na shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa ruzuku kwenye Pembejeo za kilimo, kuhimiza ushirika na masoko ya pamoja ili kuwawezesha wakulima kupata tija.
Maonesho ya nanenane mwaka 2023 kitaifa yalifungwa rasmi kanda ya nyanda za juu kusini kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya Agost 08, 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndg. Kuruthum Sadick, Mkuu wa Idara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Thadei Luoga pamoja na timu ya waataalamu wa idara ya Kilimo kutoka Halmashauri ya Mji Njombe, wanawakaribisha kuja kufanya uwekezaji kwenye kilimo cha parachichi pia wanawashukuru kwa kutembelea banda la Halmashauri ya Mji Njombe kwenye maonesho ya nanenane mwaka 2023.
Maonesho ya nanenane mwaka 2023 yalibeba Kauli Mbiu isemayo "Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula"
#dhahabuyakijaniinalipa #wekezanjombetc.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe