Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe. Erasto Mpete Mei 02,2024 alifanya ziara katika shule ya Sekondari Uwemba, iliyopo kata ya Uwemba Halmashauri ya Mji Njombe.
Katika ziara hiyo iliyolenga kuwatakia heri wanafunzi wa kidato cha sita watakaonza mtihani wa taifa Mei 06,2024, Mhe Mpete alizungumza na waalimu wa shule hiyo nakutoa pongezi kwa maendeleo mazuri ya taaluma kwenye shule hiyo.
"Niwapongeze sana kwa mafanikio kwenye matokeo, picha ya mafanikio haya ni matokeo ya umoja wenu, kazi mnayoifanya ni nzuri na mmejitoa kwa moyo, niombe muendeleze umoja na mshikamano mlio nao kwa manufaa ya shule zetu." Alisema.
Katika hatua nyingine alisisitiza waalimu kutumia njia sahihi kwenye kwenye uwasilishji na utatuzi wa changamoto zao.
"Nisisitize kufanyika vikao vya mara ni njia mojawapo ya kutatua changamoto, nishauri waalimu waalimu kuwasiliana na viongozi kwenye utatuzi wa changamoto, anzieni kwa mkuu wa shule,afisa elimu kata na ngazi nyingine."
Mhe Mpete pia aliwapongeza waalimu wote shule ya Sekondari Uwemba kwa kuwapatia zawadi ya kalamu.
Shule ya Sekondari Uwemba ina jumla ya wanafunzi 818 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, waalimu 35 na waalimu wanaojitolea 7. Shule hii Ina upungufu wa waalimu 19.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe