Kamati ya Fedha na Utawala Januari 18,2024 imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu na afya inayotekelezwa kwenye kata ya Uwemba na Ihanga Halmashauri ya Mji Njombe.
Kamati hiyo ilikagua ujenzi wa gorofa litakalokuwa na vyumba nane vya madarasa na ofisi katika shule ya Sekondari Uwemba ,ujenzi wa zahati katika kijiji cha Itipula na ujenzi wa vyumba vya madarasa ya awali katika shule ya msingi Chalima.
Utekelezaji wa miradi hiyo upo katika hatua tofauti tofauti ambapo ujenzi wa gorofa upo hatua yakumwaga jamvi,ujenzi wa zahati ya itipula na vyumba vya madarasa upo hatua ya lenta.
Baada yakukagua miradi yote wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mheshimiwa Filoteus Mligo walipongeza wananchi wa maeneo hayo kwa kuwa wadau wazuri wa maendeleo na kutoa michango yao iliyofanikisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa hatua hiyo.
Pamoja na miradi hiyo kugaramiwa na michango ya wananchi na wadau wengine wa maendeleo Serikali imetoa fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa gorofa shule ya Sekondari Uwemba ,shilingi milioni 50 kwa ajili ya ukamilishaji zahati ya Itipula na shilingi milioni 12 kwa ajili ya shule ya vyumba vya madarasa ya awali shule ya msingi Chalima.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe